Faida za Ufugaji: Kware anaweza kuokoa maisha, kumaliza umasikini
WAFUGAJI wa kuku nchini Tanzania, baadhi yao hivi sasa wamegeukia ufugaji wa ndege aina ya kware kutokana na umaarufu wa viumbe hao jamii ya ndege.
Ndege huyo mdogo amekuwa maarufu kutokana na ubora wa mayai yake yanayodaiwa kuboresha afya ya watu wenye magonjwa. Ndege hao hawahitaji uwe na eneo kubwa ili uwafuge, tofauti na kuku ambao huchukua eneo kubwa.
Viota vya kware vinaweza kuwekwa vibarazani. Mkazi wa Tegeta Kibaoni, Dar es Salaam, Suzan Magibo ni mfugaji wa kware, anasema alianza kuwafuga mwaka 2012 mwishoni kwa kuwa mama yake alikuwa na tatizo la kisukari.
Mwananchi anasema, alianza kufuga kware kwa kuwa aliambiwa mayai ya ndege huyo yana vitu mbalimbali vinavyoboresha maisha. Anasema, wakati anafikiria kufuga kware alikuwa ni mfugaji wa kuku na kanga.
“Nilishauriwa nianze kuwafuga kware kwa kuwa wanatibu maradhi mengi, niliambiwa tatizo la mama yangu linaweza kuisha kupitia mayai hayo. Nikavutiwa kwa sababu ni tiba,” anasema. Anasema kuwa, baada ya kupata maelezo kuhusu kware alikwenda kuwatafuta, hivyo kwa mara ya kwanza alichukua ndege 70 na baadaye aliongeza wengine.
Kipindi hicho anasema alinunua wa wiki mbili kwa Sh 7,000 kila mmoja. “Baada ya kuwanunua nilikaa nao wiki sita wakaanza kutaga. Nikaanza kuyatumia nilipofika trei ya tatu nikaona mwili wangu umekuwa mwepesi.
Nilikuwa na pumu hata kwenye mabanda nilikuwa siwezi kuingia. Chumbani nikipangua nguo nilikuwa napiga chafya mpaka utanihurumia,”anasema Magibo. Anasema, alipoanza kutumia mayai hayo aliona hali yake inabadilika na kuwa nzuri, tatizo la pumu hakuwa nalo tena wala upigaji wa chafya.
Magibo anasema kuwa, hata mama yake aliendelea vizuri, baada ya kutumia mayai hayo alipokuwa akipima sukari ilionekana iko vizuri. Magibo anasema, baada ya hapo akagundua kuwa ufugaji wa kware ni kazi yenye manufaa hivyo akaanza kuzalisha. Anasema, aliwazalisha kwa bidii sana wakafika 900, hivyo tatizo likawa kwenye masoko.
“Nilikuwa nakusanya mayai na kwenda kuyatotolesha, yanakaa siku 18 kwenye mashine,” anasema na kuongeza kuwa alianza kuzalisha vifaranga hivyo vya kware mwezi wa tisa mwaka juzi. Anasema alikuwa akihangaika na masoko, ilikuwa ni vigumu sana kwa siku za mwanzo, kuwaeleza watu ubora wa mayai ya kware mpaka wakuelewe.
“Nilikuwa natumia njia ya kupeleka mayai kwa wagonjwa ninapoenda kuwatembelea. Lakini kuna baba mmoja mama yake alikuwa mgonjwa alipoona nimepeleka mayai hayo aliyapiga teke akidai ni mayai ya nyoka,” anasema. Anasema, kwa wale waliokubaliana na ushauri wake waliona mafanikio, hivyo wakawa wajumbe kwa wengine.
“Haya mayai ni mazuri sana hasa yakiliwa mabichi. Yana virutubisho vingi sana, hivyo yakipikwa virutubisho hivyo vinapungua. Kuna madini ya Zinki, Omega 3 ambayo yanapatikana kwenye mafuta ya samaki, vitamin B complex. Vitamin A na D, na mengine mengi kwa hiyo ukichemsha unakuwa umepunguza virutubisho hutaweza kupata matokeo kwa haraka zaidi,” anasema.
“Watu wanafikiri kula mayai ya kware lazima waumwe kumbe hawajui ni chakula bora, kila mwanadamu anatakiwa kula,” anasema Magibo. Anasema mayai hayo ni aina ya chakula chenye alkaline. Alkaline ni kinga tosha ya matatizo ya kansa. Chembechembe za satarani haziwezi kukua kwenye alkaline.
“Ni vyema watu wote watumie hata kama wanataka kufuga wafuge kwa kuwa ni chakula bora hakichagui mzee, mtoto wala kijana,” anasema. Magibo anasema, mpaka sasa ana kware 3800, anawauza kulingana na umri. Kware mwenye umri wa siku moja anauza Sh 3,000, wa wiki moja anauza Sh 4,000, wiki mbili Sh 5,000 na wiki ya tatu Sh 8,000.
Mwezi mmoja Sh 10,000, wiki tano mpaka sita Sh 20,000 ambao wanakuwa tayari kutaga. Anaelezea kuwa wateja wao wakubwa ni wale wenye matatizo ya kiafya na wengine wanaenda kufuga wenyewe. Anasema, hajawahi kupata oda nje ya nchi ila mteja wake anayeishi Tandika, Dar es Salaam alipata mteja Uarabuni, changamoto ikawa ni kibali pamoja na namna ya upakiaji, alikwama.
“Hivi sasa nimefanya bidii kupata vifaa vya kupakia endapo nitawasafirisha. Changamoto iliyopo ni jinsi ya kuwalea, ama umeme unapokatika ni tatizo kubwa sana kwa kuwa unaweza kuta una vifaranga vya siku moja ama wiki, unapoingiza jiko la mkaa moto wake unaweza kuwa ni mkali unakuta wamekufa,” anasema.
Anasema, kware wana uwezo wa kutaga kwa miaka mitatu, pia nyama yake inaliwa kwani hivi sasa kuwa vijana wanaenda kununua ndege hao kwake na kuwapeleka hotelini. Anashauri watu kula mayai na nyama ya ndege huo, kwa kuwa ni chakula cha uhakika, virutubisho vilivyopo haviwezi kupatikana sehemu nyingine.
Magibo anashauri ili mtumiaji apate matokeo mazuri ni vema siku ya kwanza akala mayai matatu, siku ya pili matatu, siku ya tatu manne, siku ya nne matano, baada ya hapo anaendelea kula matano matano mpaka mwisho. Trei moja linahifadhi mayai 30 ambalo huuzwa Sh 30,000 ambazo ni sawa na bei ya Sh 1000 kwa kila yai.
Ofisa Mawasiliano wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Judith Mhina anasema, anashangaa kuona Tanzania imechelewa katika ufugaji wa ndege hao, kwani mwaka 1997 akiwa Malaysia alikutana na watu wanafuga ndege hao.“Hii katika nchi ile ni biashara kubwa wanatumia mayai na nyama,” anasema Mhina.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Rogers Shengoto anasema kware ni ndege ambao wamekuwa wakifugwa nchi nyingine kama Japan na India kwa miaka mingi, Wizara ina taarifa zake na inauhalalisha ufugaji huo. Shengoto anasema, uwepo wa aina hii ya ndege umeongeza changamoto kwa wizara ya kuongeza jitihada na hamasa ya ufugaji huo.
Anaeleza aina ya kware wanaofugwa kwa wingi na wafugaji nchini ni wale wanaotoka nchi za bara la Asia hasa Japan na India. “Nchi ya Japan ndiyo iliyofanya utafiti na kuchukua kware wa porini na kuanza kuwafuga na kuwaendeleza hadi kuwawezesha kufugwa.
“Ufugaji wa kware umekua na kupanuka maeneo mengine ya nchi hadi Afrika Mashariki hasa Kenya na hatimaye Tanzania,” anasema. Shengoto anasema, tafiti zilizokwisha fanyika kwenye nchi zilizoendelea hasa za bara la Asia ambazo zilianza ufugaji huo, zimeonesha kuwa mayai ya ndege hao yamesaidia kuongeza hamu ya kula, kuzuia kichefuchefu, udhaifu wa misuli na kizunguzungu.
Mayai ya ndege hao pia yameonesha kutibu matatizo kwenye mfumo wa fahamu, ukavu wa midomo, maumivu ya misuli, kunyonyoka kwa ngozi, utokaji wa nywele, kuongeza ufanisi wa kazi ya ini, magonjwa ya moyo, figo, tumbo na upungufu wa damu. “Pamoja na faida zilizoainishwa, mayai ya kware yameonesha matokeo chanya kwenye matatizo ya wagonjwa wa pumu, magonjwa ya moyo na saratani,” anasema.
Anaongeza kuwa, mayai hayo hayajaonesha tatizo linalosababisha mzio kwa watumiaji kama inavyojionesha kwa baadhi ya walaji wanaotumia mayai ya kuku na bata. Shengoto anasema, mayai ya kware yanasaidia kuyeyusha na kusambaratisha vijiwe vilivyobainika kuwepo kwenye figo, maini na mfuko wa nyongo.
Anasema, kutokana na faida zote hizo, wafugaji na wajasiriamali wameona ni vema kuchukua umuhimu wa mayai hayo kama moja ya fursa katika tasnia ya ufugaji wa kuku na aina nyingine za ndege. Mtaalamu huyo anasema kwa kuwa umuhimu wa kware na mayai yake umeonekana hapa nchini, ni vema wazalishaji wa ndege hao kama walivyo wafugaji wengine wa kuku na aina nyingine za ndege wakajitangaza na kujisajili kwenye Wizara ya Maendeleo ya Mifugo ili maeneo yao ya uzalishaji yatambulike na kusajiliwa kwa taratibu na kanuni zilizopo.
“Hii itasaidia hata kutafuta masoko ya uhakika kwa aina hii ya ndege kwa vile aina ya kware wanaofugwa sio wale wa porini ni wale waliozalishwa kwa kuingizwa mayai ya aina ya ‘Japanese quel’ kutoka nje ya nchi kwa kutumia taratibu na sheria zilizopo,” anasema.
Anasisitiza ili kuepuka uwezekano wa kuingiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, ni vema wafugaji hao wakafuata sheria, taratibu, na kanuni za Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ufugaji wa aina ya kware wa porini. Anasema, kwa kuwa aina ya kware wanaofugwa na wengi ni aina ya Japanese quail hakuna tatizo linaloweza kusababisha uzuiaji wa ufugaji huo kwani tayari hao ni aina ya kware wafugwao.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, sera ya mifugo ya mwaka 2006 inaeleza kuhamasisha ufugaji wa kuku na aina nyingine za ndege zilizoainishwa kwa kuwahasisha wafugaji kufuga. Anasema aina nyingine za ndege wafugwao zaidi kama kuku hujulikana kama ‘non –conventional domestic birds” ambao hujumuisha bata maji, njiwa, kanga, mbuni, kware na aina nyingine za ndege wafugwao.
Shengoto anasema, ili kusafirisha nje ya nchi ndege hao ni lazima kufuata taratibu na kanuni zilizopo chini wizara hiyo. Anasema kwa taarifa toka kwa wafugaji wa kware, umaarufu wa ufugaji wa ndege hao umeonekana si zaidi ya miaka mitano iliyopita nchini, inawezekana kuanzia mwaka 2010, ufugaji huo umeendelea kukua kadri siku zilivyokwenda.
Anaeleza kuwa, nchi kama Japan na India wameuchukulia ufugaji wa kware kuwa umewapa manufaa na faida kwa uchumi na walaji. “Kwa walaji na watoto wadogo mayai ya kware yanasaidia kuendeleza ubongo wa watoto wanaokua. Nyama ya kware ina kiwango kidogo cha mafuta na kwa walaji hakuna lehemu (cholesterol).
“Pia ni chakula bora kwa akina mama wanaonyonyesha na wajawazito,” anasema Shengoto. Anasema, jukumu la kubaini virutubisho vilivyopo kwenye mayai na nyama ya ndege hao ni la Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ikishirikanana Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Anasema Wizara inaandaa utaratibu wa kuwasiliana naTBS naTFDA kuhusu kufuatilia taarifa zinazosomwa kwenye matokeo ya tafiti mbalimbali duniani na Afrika kwa ujumla kuhusu manufaa hayo kwa ujumla.
Shengoto anasema, wizara imewasiliana na wadau wa ndege hao kwa kutumia wataalamu waliopo kwenye mamlaka za serikali za mitaa ili kuwatambua wazalishaji hao na kuwaelimisha kujisajii ili wafuate sheria na kanuni zilizopo.

0 comments:
Post a Comment